♫musicjinni

Miaka 7 Simba bila PATRICK MAFISANGO :Rekodi na Chanzo cha Kifo chake.

video thumbnail
#SimbaSC #Mafisango #KumbukiziYaKifo
Tarehe 9 mwezi machi mwaka 1980, alizaliwa mwamba ambaye atabaki kwenye kumbukumbu zangu na kumbukumbu za wanasoka Tanzania na barani Afrika.
Naivuta taswira yake, kisha nasAdikisha kile kilichoitwa Uzalendo, naona kivuli cha mtu nisiyemjua kwa sura, nauona mwili ukivuja jasho na miguu ikihangaika kuusaka mpira uwanjani, ghafla sura yake inajitokeZa nami nashtuka usingizini na hapo ndipo nagundua kuwa…
Ni Mrwanda alizaliwa katika mji wa Kinshasa nchini Congo, naweza kusema yeye alizaliwa kuja kuwa kiungo wa Ulinzi, kiungo mwenye kutaka mafanikio kwa kila anachokifanya.
PATRICK MUTESA MAFISANGO,Unaweza kumuita Mpambanaji lakini kule Rwanda walimuita kwa jina moja tu MZALENDO. Hakika atakumbukwa kwa mambo mengi, lakini katika soka, huyu ndiye aliyekuwa muhimili wa Simba kipindi cha msimu wa mwaka 2011 hadi 2012 kabla ya kukutwa na umauti. INNA LILLAH WAINA LILLAIH RAJIUN, MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE..
MAFISANGO Alifariki mwezi wa 5, tarehe 17 mwaka 2012 akiwa na miaka 32 pekee, hakika alifariki akiwa kijana.
Hiyo ilikuwa ni siku chache baada ya Simba kurejea kutoka nchini Sudan, katika mchezo wa Shirikisho dhidi ya Al Ahly Shandy ambapo Simba walipoteza kwa mikwaju ya penati.
Ilikuwa ni saa nne Asubuhi ya may 17, ambapo ripoti zilisambaa kuwa Mafisango amefariki Dunia baada ya gari lake kuacha njia na kupata ajali akijaribu kumkwepa Bodaboda katika eneo la keko.
ENDELEA NA MAKALA HII...... USISAHAU KU- SUBSCRIBE..

Miaka 7 Simba bila PATRICK MAFISANGO :Rekodi na Chanzo cha Kifo chake.

FIFA Yatuma Salamu Za Rambi Rambi Kwa TFF

Disclaimer DMCA