Raila Odinga ni miongoni mwa wanaoendelea kuomboleza kifo cha George Magoha |
|
Huku wakenya wakiendelea kumwomboleza aliyekuwa waziri wa elimu Profesa George Magoha aliyefariki jana kufuatia mshtuko wa moyo. Jamaa, marafiki na viongozi wa kisiasa walizuru boma lake kumfariji mkewe na Mwanawe. Miongoni mwa waliofika nyumbani kwa mwendazake ni kinara wa Azimio Raila Odinga aliyemtaja Profesa Magoha kama nguzo kuu kwa taifa aliyejitolea kuimarisha sekta ya elimu.
|