Highlights | Pan African 2-2 JKT Tanzania | U17 Club League 09/07/2023 |
|
Ilikuwa ni mechi ngumu pande zote mbili, JKT Tanzania U17 wakitumia makosa ya golikipa wa Pan African U17 kufunga magoli mawili, huku Pan nao wakitumia makosa ya mabeki wa JKT kufunga magoli mawili, moja ikiwa ni penati.
Magoli ya JKT yamefungwa na Haji Mshamu na Mohamed Omary, wakati Pan wakipata magoli yao kupitia kwa Rajabu Mohamed na Abbas Matata. Hii ni ligi kuu ya vijana U17 inayopigwa Azam Complex, Chamazi..... |