Goli ‘lililoiua’ Yanga kwenye Dimba la Samora; Lipuli FC 1-0 Yanga SC (TPL – 16/03/2019) |
|
Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, leo wamepoteza mchezo wao wa tatu msimu huu baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Lipuli FC, kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Bao pekee la wenyeji Lipuli FC limefungwa kwa ‘free-kick’ na Haruna Shamte dakika ya 20 ya mchezo. Matokeo hayo yanaifanya Yanga ibaki na alama zake 67 kileleni, huku Lipuli FC wakifikisha alama 44 na kupanda hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi. |